| |
The Fetal Period (8 Weeks through Birth)
Chapter 37 9 Weeks: Swallows, Sighs, and Stretches
|
| |
| Hatua ya tatu ya ujusu
huendelea hadi kuziliwa.
|
| Kufikai wiki ya 9
Kunyonya vidole gumba huanza
Na kijusu anaaza kumeza maji
mfukono mwake.
|
| kijitoto pia anaweza kushika,
kuelelekeza kichwa mbele na nyuma,
Kufungua na kufunga taya,
kuelekeza ulimi, na kujinyoosha.
Michocheo usoni, mikononi,
na wayoni yaweza kuhisi mguso.
Akiguswa kidogo tu mkuuni,
Kijusu ukunja ubavu na goti
na aweza kukunja vidole vya miguu.
|
| kope zimefungana kabisa sasa.
|
| Katika kooni na misulu ya sauti
hudhihirisha kuumbika
kwa vipasa sauti.
|
| kwa mtoto kike,chupa
(nyumba ya mtoto)huonekana
na chembe zalishi changa
ziitwazo "oogonia",
Yaanza kujizalishi
mfukoni mwa mayai ya uzazi.
Sehemu za nje ya uzazi zaanza kutambulika
Kama ni mume au kike.
|
Chapter 38 10 Weeks: Rolls Eyes and Yawns, Fingernails & Fingerprints
|
| |
| Kukua kwa haraka kwa mtoto
kati ya wiki 9 na 10
huongeza uzito wa mwili
zaidi ya 75%.
|
| Kufikia wiki 10,
mwasho wa sehemu ya juu ya kope
huzababisha kusunguka kwa macho.
ukielekea chini
Kijusu anaweza kwenda miayo
na kuweza kufunga na kufungua kinywa.
|
| Vijusu vingi hunyonya
vidole gumba.
Sehemu ya matumbo
katika sehemu ya ukamba
Yaaanza kurudi nyuma
ya sehemu za tumbo.
|
| Kuumbika kwa mifupa kwa mfanyiko
huitwao "osifikisheni" huimarika.
|
| Vidole vya mkono
na miguu yaanza kuumbika.
|
| Ule alama ya kipekee ya vidole
hujitokeza wiki 10 tangu kutunga mimba.
Alama hizi zaweza kutumika
kutamblisha mtu maishini yote.
|
Chapter 39 11 Weeks: Absorbs Glucose and Water
|
| |
| Katika wiki 11
Pua na midomo
Umeuumbika kabisa.
Nayo sehemu zingine za mwili,
umbo zao zitabadilika katika kila kituo
Cha ukuaji wa binadamu.
|
| Matumbo yaanza kufuta maji na sukari
zilizo mezwa na kijusu.
|
| Ijapokuwa uzazi wa mtoto
huamuliwa
wakati wa kutunga mimba,
sehemu ya nje ya sehemu za siri
yadhihirika
Kama ni mume au kike.
|
Chapter 40 3 to 4 Months (12 to 16 Weeks): Taste Buds, Jaw Motion, Rooting Reflex, Quickening
|
| |
| Kati ya wiki 11 na 12,
Uzito wa kijusu uongezeka
kwa kiwango kama 60%.
wiki ya kumi na mbili ndio mwisho
wa hatua ya kwanza
Ya hatua tatu za mimba.
|
| Uwezo wa kuonja zaimarika
Kinywani baada ya kutokea tumba.
|
| Wakati wa kuziliwa tumba
hizi za kuonjea zitapakia
ulimini peke
na kwenye paa la kinywa.
|
| Kwenda choo yaanza
mapema ya wiki 12
na kuendelea hadi wiki 6.
Ujafu hutolewayo mara ya kwanza
na kijusu kabla na baada ya kuzaliwa
yaitwa "mekoniam".
Inajumuisha
"Enzaimu" wa utumbo,
proteni, na chembe-mfu
Zilizotlewa na utumbo.
|
| Kufikia wiki ya 12
Urefu ya mikono
Utakuwa umekua na kufikia
kiwango chake cha kawaida.
Miguu huchukua muda
Kufikia kiwango chake sawa sawa.
|
| mbali na sehemu ya uti wa mgongo,
Mwili wote wa kijusu kwa sasa
yaweza kuhisi mguso kidigo.
|
| Mienendo zinazoambatana na
Jinsia
yaanza kujitokeza kwa
mara ya kwanza wakati huu.
Kwa mfano, kijusu cha kike
hufungua na kufunga kinywa
zaidi ya kitofu cha kiume.
|
| Kinyume na hali ya kujivuta
kilicho dhihirika hapo awali
midomo ikiguswa hufanya
kichwa kuelekezwa palipo toka mguso
na kufungua mdomo.
Huu huitwa mfanyiko elekezi
na huendlea baada ya kuzaliwa,
na huzaidia mtoto changa
kupata matiti ya mamaye
wakati wa kunyonya.
|
| Uso huzidi kukua
huku mafuta ya mwili ukijaza mashavu
na meno huanza kuumbika.
|
| Kufikia wiki 15, chembe
zinazo unda damu huanza kufika
a kuzalishana ndani ya
mafuta ya mifupa.
chembe-unda damu hizi
zitazalishwa kwa wengi hapa.
|
| Ijapokuwa kujinyoosha huanza,
Katika wiki ya 6,
mwanamke mja mzito huanza
kuhisi miondogo hizi za mtoto
kati ya wiki 14 n 18.
Kidesturi tokeo hili
huitwa "harakisho".
|
Chapter 41 4 to 5 Months (16 to 20 Weeks): Stress Response, Vernix Caseosa, Circadian Rhythms
|
| |
| Kufikia wiki 16,hali ya
utafiti unaohusisha
kuingizwa shindano ndani
ya kiuno cha kijusu
husababisha mkazo ya homoni
na hisia chungu au uoga
hivo kuelekea kutolewa kwa
chembe aina ya "noradrelin"
Au "norepinephrin",
kwenye damu.
Watoto wachanga na hata watu
wazima hutoa hisia hizi pia
Wanapopata mwingilio wa kutisha.
|
| Katika mfumo wa kupumua,
Ule mfreji mdogo unganishi
una karibia kumalizika
|
| Chembe-chembe maji-maji
nyeupe ya ulinzi
huitwao "vanix kaseosa"
(yaani tandabui),
hufunika kijusu kwa sasa.
tandabui huzuia ngozi
kutokana na miwasho
ya ule maji ya aminiotiki.
|
| Kuanzia wiki 19 miondogo ya kijusu,
Kupumua,
na mpigo wa moyo
huanza kufuata utaratibu
maalum kila siku
huitwao rithimu ya "Zakadiani".
|
Chapter 42 5 to 6 Months (20 to 24 Weeks): Responds to Sound; Hair and Skin; Age of Viability
|
| |
| Kufikia wiki 20 "koklea"
ambacho ni kiungo cha kusikia,
umefikia kiwango cha mtu mzima
ndani ya sehemu ilikamilika
mwa sehemu ya ndani ya masikio.
Kuanzia sasa na kuendelea,
kijusu ataanza kuhisi
Sauti ya vipimo mbali mbali.
|
| Nywele zaanza kumea kichwani.
Sehemu muundo rusu wote wa ngozi
Umekamilika,
Ukiwemo mizizi ya nywele na tezi.
|
| Kufikia wiki 21 hadi 22
tangu kutunga mimba,
mapavu hupata uwezo kidogo
ya kufuta hewa.
Umri huu huitwa umri ya "kujikimu"
kwa sababu uwezo wa kuishi
nje ya nyumba ya mtoto
huwezekana kwa baadhi
ya vijusu.
Uwezo wa utaalamu wa utibabu
huleta uwezekano ya
kudumishwa kwa maisha
ya watoto walio zaliwa
kabla ya wakati.
|
Chapter 43 6 to 7 Months (24 to 28 Weeks): Blink-Startle; Pupils Respond to Light; Smell and Taste
|
| |
| kufikia wiki 24
macho huanza kufunguka tena
Na kijusu huonyesha
Kupekupe za mstuko.
Hilo hisia husabbabishwa na tukio
kama vile sauti kubwa ya ghafla
Hutokea mapema kwa kijusu kike.
|
| utafiti umeripoti kwamba
sauti kubwa ukirudiwarudiwa
yaweza kuathiri afya ya kijusu.
Matokeo andamizi
ni pamoja mpigo wa moyo
kuongezeka kwa wakati mrefu,
Kumeza kupitia kiasi,
na tabia kubadilika ghafla.
athari za kudumu
ni pamoja kupoteza kusikia.
|
| Kiwango cha pumzi yaweza kupande juu
na kufikia pumuo 44 kwa dakika.
|
| Katika hatua ya tatu ya mimba,
kukua kwa haraka kwa ubongo
huchukua zaidi ya 50% ya nguvu
inayo tumika na kijusu.
Uzito wa ubongo huongezeka
kati ya 400 na 500%.
|
| Kufikia wiki 26
macho yatoa machozi.
Macho pia yapata kuhisi mwangaza
mapema ya wiki 27.
hali huakikisha kiwango
sawa ya mwangaza
Hufikia sehemu ya kati ya
jicho maishani kote.
|
| Vifaa vyote vinavyo takikana
Kwa mfanyiko wa kunusa
upo tayari.
Utafiti uliohusisha watoto
waliozaliwa kabla ya wakati
huonyesha uwezo wa
watoto hawa kunusu
hata mapema ya wiki 26
baada ya kutunga mimba.
Kitu kitamu kikiweka katika ule
mfuko-maji ya aminiotiki
uongeza kiwango cha
kumeza kwa kijusu.
Nayo upungufu wa kumeza,
kinyume na hali
hufuatia kuwekwa kwa
kitu chungu mle.
Sura ya uso ubadilika kwa kawaida
kutekemea machungu ama utamu.
|
| kupitia aina fulani ya mienendo
kwa kutumia miguu
Kama ile ya kutembea,
kijusu kinaweza kujipindua.
|
| ngozi ya kijusu kwa wakati huu
huonekana nyororo
kwa sababu ya nyongezeko ya
mafuta chini ya ngozi.
Mafuta hutekeleza wajibu kubwa
kwa kudumisha hali ya joto mwilini
na kuifadi nguvu baada
ya mtoto kuzaliwa.
|
Chapter 44 7 to 8 Months (28 to 32 Weeks): Sound Discrimination, Behavioral States
|
| |
| kufikia wiki 28 kijusu chaweza
kutafoutisha
Kati sauti ya juu na
sauti ya chini nyepesi.
|
| Kufikia wiki 30, mienendo
ya kupumua unakuwa wa kawaida
na hutokea 30 hadi 40% ya wakati
kwa kijusu cha kawaida.
|
| Katika miezi 4
ya mwisho wa mimba,
Kijusu huanza kuonyesha
utaratibu maalum wa mienendo
huku ukifuatiwa
na vipindi vya mapumziko.
Huu hali ya tabia
hudhihirisha ongezeko wa uwezo
kwa kiwango kikubwa
ya mifanyiko ubongoni.
|
Chapter 45 8 to 9 Months (32 to 36 Weeks): Alveoli Formation, Firm Grasp, Taste Preferences
|
| |
| Takriban wiki 32
vipenyesi vya hewa uyavuni
( "alveoli")
au chembe za mifuko za hewa
huanza kuumbika.
Yataendelea kuzalisha hata
miaka 8 baada ya kuzaliwa mtoto.
|
| Katika wiki ya 35 kijusu
anaweza kushika imara
kwa mkono.
|
| Kijusu akizoeshwa
aina fulani ya vionjo
huonekana kupelekea mapendeleo
ya aina fulani baada ya kuzaliwa.
Kwa mfano, kijusu
ambacho mamaye alitumia "anis"
Kiungo kinacho kipa "likoris"
Onjo lake,
alionyesha kupendelea "anis"
baada ya kuzaliwa.
Watoto ambayo hawa kupata "anis"
kabla ya kuzaliwa hawakupenda.
|
Chapter 46 9 Months to Birth (36 Weeks through Birth)
|
| |
| Kijusu huanza kusababisha
utungu ya uzazi
kwa kutoa kwa kiwango kikubwa cha
homoni yaitwao estrojeni
na hivo kuanzisha hali kutoka
kwa kijusu na kuwa mtoto changa.
utungu ya uzazi husababishwa
na mfutano wa chumba cha mtoto,
na kusababisha kuzaliwa kwa mtoto.
|
| Kuanzia kutunga mimba hadi
kuzaliwa kwa mtoto na baadaye,
Kukua kwa binadamu ni mfanyiko
uendeleayo bila kikomo na ngumu.
Matokeo mapya ya utafiti kuhusu
mfanyiko huu wa kustajabisha
huendelea kudhihirisha
athari za ukuaji wa kijusu
katika afya ya binadamu
maishani kote.
Jinsi ufahamu wetu wa ukuaji
wa kijusu unavyo zidi kuimarika
ndivyo uwezo wetu wa kuimarisha
afya unavoy zidi kuwa bora zaidi
kabla na baada ya mtu kuzaliwa.
|