Skip Navigation
The Endowment for Human Development
The Endowment for Human Development
Improving lifelong health one pregnancy at a time.
Donate Now Get Free Videos

Multilingual Illustrated DVD [Tutorial]

The Biology of Prenatal Development
BIOLOJIA YA UKUAJI WA MTOTO TUMBONI

.Swahili


National Geographic Society This program is distributed in the U.S. and Canada by National Geographic and EHD. [learn more]

Choose Language:
Download English PDF  Download Spanish PDF  Download French PDF  What is PDF?
 

The Fetal Period (8 Weeks through Birth)

Chapter 37   9 Weeks: Swallows, Sighs, and Stretches

Hatua ya tatu ya ujusu huendelea hadi kuziliwa.

Kufikai wiki ya 9 Kunyonya vidole gumba huanza Na kijusu anaaza kumeza maji mfukono mwake.

kijitoto pia anaweza kushika, kuelelekeza kichwa mbele na nyuma, Kufungua na kufunga taya, kuelekeza ulimi, na kujinyoosha.

Michocheo usoni, mikononi, na wayoni yaweza kuhisi mguso.

Akiguswa kidogo tu mkuuni, Kijusu ukunja ubavu na goti na aweza kukunja vidole vya miguu.

kope zimefungana kabisa sasa.

Katika kooni na misulu ya sauti hudhihirisha kuumbika kwa vipasa sauti.

kwa mtoto kike,chupa (nyumba ya mtoto)huonekana na chembe zalishi changa ziitwazo "oogonia", Yaanza kujizalishi mfukoni mwa mayai ya uzazi.

Sehemu za nje ya uzazi zaanza kutambulika Kama ni mume au kike.

Chapter 38   10 Weeks: Rolls Eyes and Yawns, Fingernails & Fingerprints

Kukua kwa haraka kwa mtoto kati ya wiki 9 na 10 huongeza uzito wa mwili zaidi ya 75%.

Kufikia wiki 10, mwasho wa sehemu ya juu ya kope huzababisha kusunguka kwa macho. ukielekea chini

Kijusu anaweza kwenda miayo na kuweza kufunga na kufungua kinywa.

Vijusu vingi hunyonya vidole gumba.

Sehemu ya matumbo katika sehemu ya ukamba Yaaanza kurudi nyuma ya sehemu za tumbo.

Kuumbika kwa mifupa kwa mfanyiko huitwao "osifikisheni" huimarika.

Vidole vya mkono na miguu yaanza kuumbika.

Ule alama ya kipekee ya vidole hujitokeza wiki 10 tangu kutunga mimba. Alama hizi zaweza kutumika kutamblisha mtu maishini yote.

Chapter 39   11 Weeks: Absorbs Glucose and Water

Katika wiki 11 Pua na midomo Umeuumbika kabisa. Nayo sehemu zingine za mwili, umbo zao zitabadilika katika kila kituo Cha ukuaji wa binadamu.

Matumbo yaanza kufuta maji na sukari zilizo mezwa na kijusu.

Ijapokuwa uzazi wa mtoto huamuliwa wakati wa kutunga mimba, sehemu ya nje ya sehemu za siri yadhihirika Kama ni mume au kike.

Chapter 40   3 to 4 Months (12 to 16 Weeks): Taste Buds, Jaw Motion, Rooting Reflex, Quickening

Kati ya wiki 11 na 12, Uzito wa kijusu uongezeka kwa kiwango kama 60%.

wiki ya kumi na mbili ndio mwisho wa hatua ya kwanza Ya hatua tatu za mimba.

Uwezo wa kuonja zaimarika Kinywani baada ya kutokea tumba.
Wakati wa kuziliwa tumba hizi za kuonjea zitapakia ulimini peke na kwenye paa la kinywa.

Kwenda choo yaanza mapema ya wiki 12 na kuendelea hadi wiki 6.

Ujafu hutolewayo mara ya kwanza na kijusu kabla na baada ya kuzaliwa yaitwa "mekoniam". Inajumuisha "Enzaimu" wa utumbo, proteni, na chembe-mfu Zilizotlewa na utumbo.

Kufikia wiki ya 12 Urefu ya mikono Utakuwa umekua na kufikia kiwango chake cha kawaida. Miguu huchukua muda Kufikia kiwango chake sawa sawa.

mbali na sehemu ya uti wa mgongo, Mwili wote wa kijusu kwa sasa yaweza kuhisi mguso kidigo.

Mienendo zinazoambatana na Jinsia yaanza kujitokeza kwa mara ya kwanza wakati huu. Kwa mfano, kijusu cha kike hufungua na kufunga kinywa zaidi ya kitofu cha kiume.

Kinyume na hali ya kujivuta kilicho dhihirika hapo awali midomo ikiguswa hufanya kichwa kuelekezwa palipo toka mguso na kufungua mdomo. Huu huitwa mfanyiko elekezi na huendlea baada ya kuzaliwa, na huzaidia mtoto changa kupata matiti ya mamaye wakati wa kunyonya.

Uso huzidi kukua huku mafuta ya mwili ukijaza mashavu na meno huanza kuumbika.

Kufikia wiki 15, chembe zinazo unda damu huanza kufika a kuzalishana ndani ya mafuta ya mifupa. chembe-unda damu hizi zitazalishwa kwa wengi hapa.

Ijapokuwa kujinyoosha huanza, Katika wiki ya 6, mwanamke mja mzito huanza kuhisi miondogo hizi za mtoto kati ya wiki 14 n 18. Kidesturi tokeo hili huitwa "harakisho".

Chapter 41   4 to 5 Months (16 to 20 Weeks): Stress Response, Vernix Caseosa, Circadian Rhythms

Kufikia wiki 16,hali ya utafiti unaohusisha kuingizwa shindano ndani ya kiuno cha kijusu husababisha mkazo ya homoni na hisia chungu au uoga hivo kuelekea kutolewa kwa chembe aina ya "noradrelin" Au "norepinephrin", kwenye damu. Watoto wachanga na hata watu wazima hutoa hisia hizi pia Wanapopata mwingilio wa kutisha.

Katika mfumo wa kupumua, Ule mfreji mdogo unganishi una karibia kumalizika

Chembe-chembe maji-maji nyeupe ya ulinzi huitwao "vanix kaseosa" (yaani tandabui), hufunika kijusu kwa sasa. tandabui huzuia ngozi kutokana na miwasho ya ule maji ya aminiotiki.

Kuanzia wiki 19 miondogo ya kijusu, Kupumua, na mpigo wa moyo huanza kufuata utaratibu maalum kila siku huitwao rithimu ya "Zakadiani".

Chapter 42   5 to 6 Months (20 to 24 Weeks): Responds to Sound; Hair and Skin; Age of Viability

Kufikia wiki 20 "koklea" ambacho ni kiungo cha kusikia, umefikia kiwango cha mtu mzima ndani ya sehemu ilikamilika mwa sehemu ya ndani ya masikio. Kuanzia sasa na kuendelea, kijusu ataanza kuhisi Sauti ya vipimo mbali mbali.

Nywele zaanza kumea kichwani.

Sehemu muundo rusu wote wa ngozi Umekamilika, Ukiwemo mizizi ya nywele na tezi.

Kufikia wiki 21 hadi 22 tangu kutunga mimba, mapavu hupata uwezo kidogo ya kufuta hewa. Umri huu huitwa umri ya "kujikimu" kwa sababu uwezo wa kuishi nje ya nyumba ya mtoto huwezekana kwa baadhi ya vijusu. Uwezo wa utaalamu wa utibabu huleta uwezekano ya kudumishwa kwa maisha ya watoto walio zaliwa kabla ya wakati.

Chapter 43   6 to 7 Months (24 to 28 Weeks): Blink-Startle; Pupils Respond to Light; Smell and Taste

kufikia wiki 24 macho huanza kufunguka tena Na kijusu huonyesha Kupekupe za mstuko. Hilo hisia husabbabishwa na tukio kama vile sauti kubwa ya ghafla Hutokea mapema kwa kijusu kike.

utafiti umeripoti kwamba sauti kubwa ukirudiwarudiwa yaweza kuathiri afya ya kijusu. Matokeo andamizi ni pamoja mpigo wa moyo kuongezeka kwa wakati mrefu, Kumeza kupitia kiasi, na tabia kubadilika ghafla. athari za kudumu ni pamoja kupoteza kusikia.

Kiwango cha pumzi yaweza kupande juu na kufikia pumuo 44 kwa dakika.

Katika hatua ya tatu ya mimba, kukua kwa haraka kwa ubongo huchukua zaidi ya 50% ya nguvu inayo tumika na kijusu. Uzito wa ubongo huongezeka kati ya 400 na 500%.

Kufikia wiki 26 macho yatoa machozi.

Macho pia yapata kuhisi mwangaza mapema ya wiki 27. hali huakikisha kiwango sawa ya mwangaza Hufikia sehemu ya kati ya jicho maishani kote.

Vifaa vyote vinavyo takikana Kwa mfanyiko wa kunusa upo tayari. Utafiti uliohusisha watoto waliozaliwa kabla ya wakati huonyesha uwezo wa watoto hawa kunusu hata mapema ya wiki 26 baada ya kutunga mimba.

Kitu kitamu kikiweka katika ule mfuko-maji ya aminiotiki uongeza kiwango cha kumeza kwa kijusu. Nayo upungufu wa kumeza, kinyume na hali hufuatia kuwekwa kwa kitu chungu mle. Sura ya uso ubadilika kwa kawaida kutekemea machungu ama utamu.

kupitia aina fulani ya mienendo kwa kutumia miguu Kama ile ya kutembea, kijusu kinaweza kujipindua.

ngozi ya kijusu kwa wakati huu huonekana nyororo kwa sababu ya nyongezeko ya mafuta chini ya ngozi. Mafuta hutekeleza wajibu kubwa kwa kudumisha hali ya joto mwilini na kuifadi nguvu baada ya mtoto kuzaliwa.

Chapter 44   7 to 8 Months (28 to 32 Weeks): Sound Discrimination, Behavioral States

kufikia wiki 28 kijusu chaweza kutafoutisha Kati sauti ya juu na sauti ya chini nyepesi.

Kufikia wiki 30, mienendo ya kupumua unakuwa wa kawaida na hutokea 30 hadi 40% ya wakati kwa kijusu cha kawaida.

Katika miezi 4 ya mwisho wa mimba, Kijusu huanza kuonyesha utaratibu maalum wa mienendo huku ukifuatiwa na vipindi vya mapumziko. Huu hali ya tabia hudhihirisha ongezeko wa uwezo kwa kiwango kikubwa ya mifanyiko ubongoni.

Chapter 45   8 to 9 Months (32 to 36 Weeks): Alveoli Formation, Firm Grasp, Taste Preferences

Takriban wiki 32 vipenyesi vya hewa uyavuni ( "alveoli") au chembe za mifuko za hewa huanza kuumbika. Yataendelea kuzalisha hata miaka 8 baada ya kuzaliwa mtoto.

Katika wiki ya 35 kijusu anaweza kushika imara kwa mkono.

Kijusu akizoeshwa aina fulani ya vionjo huonekana kupelekea mapendeleo ya aina fulani baada ya kuzaliwa. Kwa mfano, kijusu ambacho mamaye alitumia "anis" Kiungo kinacho kipa "likoris" Onjo lake, alionyesha kupendelea "anis" baada ya kuzaliwa. Watoto ambayo hawa kupata "anis" kabla ya kuzaliwa hawakupenda.

Chapter 46   9 Months to Birth (36 Weeks through Birth)

Kijusu huanza kusababisha utungu ya uzazi kwa kutoa kwa kiwango kikubwa cha homoni yaitwao estrojeni na hivo kuanzisha hali kutoka kwa kijusu na kuwa mtoto changa.

utungu ya uzazi husababishwa na mfutano wa chumba cha mtoto, na kusababisha kuzaliwa kwa mtoto.

Kuanzia kutunga mimba hadi kuzaliwa kwa mtoto na baadaye, Kukua kwa binadamu ni mfanyiko uendeleayo bila kikomo na ngumu. Matokeo mapya ya utafiti kuhusu mfanyiko huu wa kustajabisha huendelea kudhihirisha athari za ukuaji wa kijusu katika afya ya binadamu maishani kote.

Jinsi ufahamu wetu wa ukuaji wa kijusu unavyo zidi kuimarika ndivyo uwezo wetu wa kuimarisha afya unavoy zidi kuwa bora zaidi kabla na baada ya mtu kuzaliwa.


Add a Comment

Your Name: Log In 3rd-party login: Facebook     Google     Yahoo

Comment: